Thursday, November 18, 2010

NAKUPA POLE HUKO GEREZANI.

Naandika kwa masikitiko makubwa, kwa hatua ambazo waamerika walizichukua kumtuhumu mtanzania na kisha kumfungulia mashitaka dhidi ya mabomu yaliyosababisha vifo vya watanzania na wakenya katika matukio mawili tofauti yaliyotokea kwa wakati unaokaribiana julai1998.

Mtuhumiwa kijana wetu wa kitanzania ,ambaye hivi sasa ni mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha Ahamed  Khalifan  Ghailan huko nchini Amerika nakupa pole! Adhabu dhidi yako haikuzingatia ushahidi timilifu  usio na shaka yaonekana umekiuka misingi ya haki katika  uendeshaji wa mashtaka ya jinai ambapo upande wa mashitaka unapaswa kudhibitisha pasipo  kivuli cha mashaka ili mshtakiwa atiwe hatiani.

Ni dhahiri hukumu ya mtanzania huyu imetolewa kwa lengo la chuki inayotokana na  mawazo ya kulipiza kisasi dhidi ya mtandao wa AL Qaeda ,ambapo hadi hivi sasa wanamsaka  usiku na mchana na kwa udi na uvumba gaidi Osama kama nchi za magharibi zinavyomuita bila mafanikio!

Poleni wakubwa mmezidiwa  kete na maarifa hadi hivi leo hali ni tete mmeshindwa kumkamata gaidi namba moja mwenye kumiliki huo mtandao tata unaowasumbua.

Kwa maoni yangu kumtia hatiani Ghailani kwa kusababisha vifo vya watu 281 mwaka 1998  huko nchini Marekani ni uonevu,  waliopoteza ndugu na wapendwa  wao ni wakenya na watanzania, kwa nini mtuhumiwa asingalishtakiwa nchini Kenya au Tanzania mahali ambapo ndipo matukio yalipotokea?

Kutokana na utetezi wa mshtakiwa  Ghailan  akijitetea kwa kutumia wakili wake alidai siku ya tukio hakuwepo nchini Kenya wala Tanzania, alidai alikuwa safarini  nchini Pakistan. Shauri lake lilitakiwa liangaliwe kwa kina na majaji wawe huru huku wazingatie utetezi wa kutokuwepo (ALIBI) na  siyo kuangalia na kuzingatia maslahi ya wamerikani juu ya kesi hiyo.

Penginepo hukumu dhidi yake imepikwa ili kuwalinda wakubwa, kutokana na uzembe wa kutokuwa na ulinzi wa kutosha katika balozi zilizoko jijini Nairobi na Dar-es-salaam.kwa wakati huo!! Hali ya ulinzi ilivyo kwenye balozi inatia aibu kwa mnyonge mwana harakati huyo kuthibitika kwamba alihusika dhidi ya  tukio hilo.

Sheria ni sheria ina pande mbili ya kutiwa hatiani ama kuachiliwa, kilichobaki sisi wanaharakati wa masuala ya  haki za binadamu tupo nyuma yakowewe mfungwa wa ughaibuni tutapiga kelele nakukuombea makanisani na miskitini iwapo ni kweli haukuhusika kwa namna moja ama nyingine katika tukuo hilo!  Iko siku milango ya gereza itakuwa wazi utaachiliwa, Mungu anaendelea kubariki huko huko ulipo kifungoni.

Lakini, iwapo nafsi yako inakusuta kwa kushiriki kimawazo ama kula njama hatimaye ukasababisha vifo vya  ndugu zetu wakenya na watanzania wasio na hatia ,adhabu ulipewa haitoshi ulipashwa kuhukumiwa kifo   Kwani .dawa ya moto ni moto na mwenye kuua kwa upanga naye ni sharti afe kwa upanga!.

KWA HERI.......DUMU KATIKA MAOMBI...

No comments:

Post a Comment