Tuesday, November 16, 2010

Habari mpya

Leo ni siku ya pili tangu tuanze kujifunza namna bora ya kutumia internet  kwa ufanisi wa vyombo vya habari hapa nchini na ulimwenguni pote ili kwenda sambamba na wakati huu wa kutumia njia za mitandao ili kupunguza gharama na kujifunza mengi.

 Elimu hii imeniwezesha mimi binafsi,kujua ni jinsi gani naweza kurahisisha kazi ya kupokea,kuandika, kuhariri kisha kuipeleka habari kwenye chombo husika kwa wakati ili kiweze kuwafikia wasomaji ama wasikilizaji kwa wakati muafaka.

Elimu niliyoipata imewezesha kupata uwezo wa kusoma magazeti mbalimbali kwa njia ya mtandao.Hivyo ni dhahiri nimepanua wigo na uwezo wangu wa kuwa na vyanzo vingi vya habari vikiwemo vyanzo vya mitandao mbalimbali mfano wikipedia, goggle na bloggers.

Mbali ya kusoma magazeti ya vyombo vya habari yanayopatikana hapa nchini napendelea kusoma magazeti ya Daily Nation ya Kenya kwa sababu  habari  zake ni  nyingi zinazoandikwa kwa umakini na  zilizofanyiwa utafiti wa kina.

Napendelea kusoma magazeti ya kiswahili ya  Mwanahalisi na Raia mwema ya Tanzania   kutokana na ukweli kwamba ni ya uchambuzi.

Vilevile nasoma magazeti ya kampuni ya Business Times kwa  lengo la kuelewa yaliyojili ndani ya magazeti hayo.Magazeti ya kampuni hii yanapatikana ndani ya tovuti.

Mwisho nawashauri wanahabari tujifunze kwa makini taaluma hii ya habari inayoenda na mabadiliko kasi ya sayansi  na teknojia.

No comments:

Post a Comment